Ibraah’s Bado ( Magufuli ) Lyrics

34

Siamini ndoto zimeishia njiani Baba shupavu we huko tena duniani Na ulituahidi utafikisha taifa Pale pale baba Magu

Nyuso ya taifa imetawala huzuni Kukurudisha ndo hatuwezi jamani Na kazi ya Mungu huwezi pinga abadani Ayee ayee baba Magu

Baba umeondoka taifa umemuachia mama Na hatuna cha kufanya tunalia wana Wote twasema bye bye Twasema bye bye, hatuna budi

Baba umeondoka taifa umemuachia mama Na hatuna cha kufanya tunalia wana Wote twasema bye bye Twasema bye bye, hatuna budi

Nikitazama taifa ulivyojenga hata siamini Eti Magu umeondoka kweli haingii akilini Ha roho inaniuma mimi baba, baba Baba Kikwete analia hadi na Baba mwinyi Na Kassim Majaliwa bado hatuamini Kama umetutoka baba baba

Ila baba, bado, bado Bado hatuamini bado, bado, bado Kama kweli we umetangulia, bado Oh kuamini bado inakuwa ngumu, bado bado Bado, bado bado, bado hatuamini bado

Maneno yako yatakumbukwa daima we baba shupavu Ulizo amini wajane hadi walemavu Magufuli we ulijaa wema Ulikuwa ni mwingi wa huruma

Haya sawa tuishi bila matabaka, ni wewe Elimu bure kusoma bila mipaka, ni wewe Ulideal na wala rushwa waiba sadaka, ni wewe Ni wewe na ni wewe

Na wamachenga tufanye kazi popote, ni wewe  Ulisimama baba we ulitutetea Leo twatokwa machozi twakulilia  Ni wewe ni wewe

Bado, bado baba, bado, bado Bado hatuamini bado, bado, bado Kama kweli we umetangulia, bado Oh kuamini bado inakuwa ngumu, bado bado Oh bado hatuamini bado


Ibraah’s Bado ( Magufuli ) Lyrics.For More Article Visit Anxiousfrogs

Comments are closed.