Rose Muhando’s Mapambio Lyrics

55

Ukipata mia mbili shukuru Mungu Hio ndio riziki yako Kaa chini utulie imba mapambio Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa

Wewe tulia mshukuru Mungu Hio ndio riziki yako Kaa chini utulie imba mapambio Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa

Yatakutoa roho Wacha kwenda mbio mbio Usishindane na huyo Wewe nenda pole pole, pole pole Maisha ni pole pole, pole pole

Mungu ameumba dunia riziki mafungu saba Wewe imba mapambio Pengine la kwanza na la pili si lako La kwako saba we, tulia imba mapambio

Wacha kutamani vitu vya wengine Vinaumiza moyo Wewe imba mapambio Ridhika na ulicho nacho

Wewe tulia mshukuru Mungu Hio ndio riziki yako Kaa chini utulie imba mapambio Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa

Ya watu yatakutoa nyongo Unataka mapesa kama ya fulani utatoa wapi? Wewe imba mapambio Wataka utajiri kama wa fulani hujui alipataje? Wewe imba mapambio

Fulani ana utajiri na hujui agano lako Kama itakutoa nyongo Mumeo kipato chake ni buku Hafanani na fulani, mwombee imba mapambio Wewe imba mapambio, shukuru Mungu Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa

Ukipata mia mbili shukuru Mungu Hio ndio riziki yako Kaa chini utulie imba mapambio Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa Yatakutoa roho

Wataka mrembo wa gharama kama Wema Sepetu Kwa kipato cha Harmo Rapa we yatakutoa nyongo Chunga atakutoa roho

Mrembo ana stage ya pizza Kipato chako miguu ya kuku, chunga atakutoa roho Wewe imba mapambio, shukuru Mungu Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa

Dunia ina mambo, ina mambo Vituko na vijambo na vijambo Siri nyumba ya mgongo, ya mgongo Usishindane na huyo

Ukipata mia mbili shukuru Mungu Hio ndio riziki yako Kaa chini utulie imba mapambio Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa

Wewe tulia mshukuru Mungu Hio ndio riziki yako Kaa chini utulie imba mapambio Kunywa maji ukalale mengine yatakutesa

Rose Muhando’s Mapambio Lyrics.For More Article Visit Anxiousfrogs

Comments are closed.